✍🏾NAKUNGOJA ni Wimbo wa Saburi uliozaliwa baada ya Kukutana na mtumishi wa MUNGU Kutoka Nchini Kenya @evelynwanjiru aliemsubiri Mungu kwa habari ya Uzao takribani miaka 10
✍🏾Kwa kadiri ya Saburi na tumaini liliumbika ndani ya mtumishi wa MUNGU huyu ndipo Roho Mtakatifu Akanijalia Kuimba Wimbo huu
✍🏾Na kwa sasa Mungu amempatia mtoto kwa wakati maaalumu kabisa na Amemfanyia Kicheko Kama Ilivyokuwa kwa Sarah
✍🏾Ni maomhi yangu kwamba Mungu akafanye na kwako na akaimarishe saburi yako kipindi unapomngoja Yeye akakujibu kama Alivyomjibu Mtumishi wake hatimaye ukawe ushuhuda Katika maisha yako🙌🔥
Isaya 30:18
Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
MUNGU AKUKUMBUKE 🙌